Connect with us

Na Fredrick Nwaka,

Dar es Salaam. Klabu ya Simba kesho itakutana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam nchini Tanzania ambako itazungumza kuhusu mchakato wa zabuni za ununuzi wa hisa.

Klabu hiyo kubwa nchini Tanzania imekuwa katika mchakato wa kubadili mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo kuwa wa hisa.

Ofisa Mawasiliano wa Simba Haji Manara amesema mkutano huo ni muhimu kutokana na mazingira ya sasa.

“Tuko kwenye mchakato muhimu na kesho tutazungumza kuhusu namna zabuni zetu zitakvyokwenda,”alisema Manara.

Wakati huohuo Manara alisema klabu yake iko kwenye maandalizi kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar utakaochezwa wiki ijayo.

“Tunawaheshimu Mtibwa lakini tunahitaji alama tatu kweny mchezo huo, kila mechi ni fainali kwetu,”alisema Manara.

More in African Football