Connect with us

Mchezo wa mzunguko wa kumi na moja wa Ligi Kuu baina ya Simba na Lipuli uliopangwa kuchezwa Uwanja Azam Complex, sasa utachezwa Uwanja wa Uhuru hapo kesho.

Mchezo huo utakuwa wa mwisho kwa Simba kabla ya wachezaji wake kujiunga na Timu ya Taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ inayiotarajia kwenda nchini Kenya kwenye michuano ya Kombe la Chalenji.

Akizungumza na mtandao huu Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas amesema mchezio huo umerudishwa Uwanja wa Uhuru kwa sababu utakuwa wazi.

“Serikali ilisema kutakuwa na matumizi lakini tumeambiwa utakuwa wazi Jumapili, hivyo tumeurudisha mchezo huo Uwanja wa Uhuru,”amesema Lucas.

Kocha wa Simba Joseph Omog amesema timu yake inahitaji alama tatu ili kuendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu.

Hata hivyo mchezo huo hautakuwa rahisi kwa sababu Lipuli inayofundishwa na mchezaji wa zamani wa Simba, Seleman Matola ambaye amepania kuizamisha timu yake ya zamani.

African journalist with passion of football reporting.Also i love politics

More in