Connect with us

Mabingwa watetezi wa taji la CECAFA miongoni mwa vlabu ya Afrika Mashariki Azam FC ya Tanzania, inachuana na Simba FC pia ya Tanzania katika fainali ya michuano ya mwaka huu.

Mechi hii itachezwa saa 10 jioni katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam nchini Tanzania.

Azam FC ilifika katika hatua hiyo baada ya kuifunga Gor Mahia mabao 2-0 katika mechi ya nusu fainali wiki hii.

Nayo Simba, iliishinda Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) kutoka Zanzibar bai 1-0 na kuingia katika fainali.

Simba inakwenda katika fainali hii ikiwa na rekodi ya kushinda mataji sita ya CECAFA na hivyo kuwa klabu bora katika michuano hii.Mara ya mwisho kushinda ilikuwa ni mwaka 2002.

Timu nyingine ambazo zimeshinda mataji haya mara tano ni pamoja na AFC Leopards ya Kenya, Yanga ya Tanzania pamoja na Gor Mahia na Tusker zote kutoka Kenya.

Mshindi atapata Dola za Marekani 30,000 mshindi wa pili Dola, 20,000 na mshindi wa tatu Dola 10,000. Fedha hizo zimetolewa na rais wa Rwanda Paul Kagame.

Mechi ya kutafuta nafasi ya tatu ni kati ya mabingwa wa Kenya Gor Mahia na JKU kuanzia saa nane mchana saa za Afrika Mashariki.

 

More in East Africa