Connect with us

Na Fredrick Nwaka,

Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania imesema mchezo wa Ligi Kuu baina ya Simba na Yanga hautachezwa Uwanja wa Taifa kwa sababu uwanja huo upo kwenye matengenezo.

Simba na Yanga ambao ni wapinzani wa jadi kwenye soka la Tanzania watavaana Oktoba 28 na wadau wa soka wameanza kujiulza mchezo huo utachezwa kwenye uwanja gani.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na michezo Dr Harrison Mwakyembe amesema mchezo huo hautachezwa Uwanja wa Taifa.

“Uwanja ule unefungwa na kwa mujibu wa mkandarasi matengenezo yatachukua miezi mitatu, haitawezekana kwa Simba na Yanga kucheza pale,”amesema Mwakyembe ambaye pia ni mbunge wa Kyela, Mkoani Mbeya.

Kauli hiyo ya waziri mwakyembe inamaliza uvumi na ni wazi kuwa mechi hiyo itachezwa kwenye Uwanja wa Uhuru.

More in