Connect with us

Miamba ya soka nchini Tanzania itashuka uwanjani kesho kuumana katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara unaosubiriwa kwa hamu na ghamu na mashabiki wa soka nchini kote na katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Katika mchezo huo Simba wanaingia uwanjani wakiwa wanaongoza ligi baada ya kujikusanyia pointi 59 ikicheza michezo 25 wakati Yanga wana pointi 48 wakiwa nafasi ya pili baada ya kucheza michezo 23.

Timu zote mbili ziliweka kambi Mkoani Morogoro na tayari zimesharejea jijini Dar es salaam kwa mchezo huo utakaochezeshwa na mwamuzi wa kimataifa Emanuel Mwandembwa.

Ofisa Habari na Mawasiliano wa yanga, Dismas Ten amesema timu yake imejiandaa kikamilifu kwa ajili ya mchezo huo ikidhamiria kupata alama tatu.

“Mchezaji pekee atakayekosa mchezo huo ni Donald Ngoma lakini wachezaji wote wako tayari kwa mchezo, tuinaomba waamuzi wachezeshe kwa kuzingatia sheria 17 za soka,”amesema Ten, alipozungumza na vyombio vya habari jana Ijumaa.

Kwa uoande wake Ofisa Habari na Mawasiliano wa Simba,Haji Manara ameweka wazi kwamba Simba na Yanga si mahasimu bali ni watani wa jadi na kusema mpira una matokeo matatu.

“Tunatambua Yanga ni timu kubwa kama sisi tunaiheshimu, tunaingia uwanjani kutafuta ushindi, nawao,mba mashabiki wa Simba wajitokeze kwa wingi uwanjani kuishnagilia timu yao,”amesema Manara.

Tayari tiketi za mchezo huo zinaendelea kuuzwa ambapo VIP A ni shilingi 30,000,VIP B na C 20,000 na Mzunguko(Jukwaa la rangi ya Chungwa,Kijani na Bluu) 7,000.

Tiketi zinapatikana kupitia Selcom.

Katika hatua nyingine Shirikisho la Soka Tanzania TFF limemtaja Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Paul Makonda kuwa atakuwa mgeni rasmi wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara utakaowakutanisha Simba na Yanga utakaochezwa Jumapili Aprili 29,2018 Uwanja wa Taifa Dar Es Salaam.

Ndugu Makonda atawaongoza maelfu ya mashabiki wa mpira wa miguu watakaojitokeza kweye Uwanja wa Taifa kushuhudia mchezo huo namba 178 utakaoanza saa 10 jioni.

 

 

African journalist with passion of football reporting.Also i love politics

More in East Africa