Connect with us

Na Fredrick Nwaka,

Dar es Salaam. Simba imeanza kwa kasi Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa kuifunga Ruvu Shooting mabao 7-0.

Mchezo huo wa uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru ulitawaliwa kwa muda mrefu na Simba.

Mshambuliaji raia wa Uganda Emanuel Okwi amefunga mabao manne huku mabao mengine yakifungwa na Erasto Nyoni, Shiza Kichuya na Juma Luizio.

Mechi nyingine zilizochezwa leo Azam imeishinda Ndanda kwa bao 1-0, Prisons imeichapa Njombe Mji bao 1-0 wakati Mwadui ya Shinyanga imeishinda Singida United kwa mabao 2-1.

Mtibwa Sugar pia imeshinda mchezo wa kwanza kwa bao 1-0 dhidi ya Stand United.

Ligi hiyo itaendelea kesho ambapo bingwa mtetezi Yanga atacheza na Lipuli iliyopanda daraja

More in African Football