Connect with us

Na Fredrick Nwaka,

Dar es Salaam. Matatu matatu yaliyofungwa na Emmanuel Okwi na John Bocco yameipa Simba ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mwadui.

Mashabiki wa Simba walikuwa wakicheka muda wote wa mchezo walipoishuhudia timu yao ikitakata uwanjani hapo.

Okwi alifunga mabao mawili kipindi cha kwanza na Bocco alifunga bao kipindi cha pili na kukamilisha ushindi wa pili wa Simba katika michezo mitatu ya Ligi Kuu.

Hata hivyo Simba itajilaumu baada ya kupoteza nafasi nyingi kupitia Bocco na Okwi ambao wangeweza kufunga mabao mengi kama wangekuwa makini.

Kwa matokeo hayo Simba imefikisha pointi saba na kupanda hadi nafasi ya pili nyuma ya Mtibwa Sugar inayoongoza kwa kuwa na pointi tisa.

Wiki ijayo Simba itasafiri kwenda Mwanza kupambana na Mbao FC.

More in