Connect with us

Klabu ya Simba imefanikiwa kumsajili Gor Mahia ya Kenya, Meddie Kagere.

Ripoti kutoka Tanzania zilizomnukuu Meneja wa mchezaji huyo Patrick Gakumba akisema kwa asilimia kubwa kila kitu kimekamilika.

“Tumekubaliana na Simba, dili limekamilika, amesaini na kilichobaki ni Simba kumtangaza hadharani,”amesema Gakumba.

Gor Mahia imemsajili Erisa Ssekisambu ili kuziba nafasi ya Meddie Kagere.

Mchezaji huyo alifanya vyema kwenye michuano ya Sports Pesa na amekuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Gor Mahia ambacho kinashiriki hatua ya makundi ya taji la shirikisho Afrika.

Awali, ilitajwa mchezaji huyo alitajwa kuwaniwa na Yanga lakini Simba iliingilia kati.

Kagere ni mnyarwanda ambaye alizaliwa nchini Uganda.

African journalist with passion of football reporting.Also i love politics

More in