Connect with us

Mwaka 2017 unatia nanga leo saa sita usiku kwa saaa za Afrika mashariki lakini klabu ya Simba yenye maskani yake mtaa wa Msimbazi Jijini Dar es Salaam, inamaliza mwaka kwa kuwa kileleni mwa Ligi Kuu.

Simba ambayo hivi karibuni ilimfuta kazi Kocha wake Joseph Omog jana iliichapa Ndanda FC ya Mtwara katika mechi ya Ligi Kuu iliyochezwakwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mkoani Mtwara, Kusini mwa Tanzania.

Ushindi wa Simba uliifanya ifikishe alama 26 sawa na Azamn lakini inasalia kileleni kutokana na kuwa na idadi ya mabao mengi ya kufunga. Simba imefunga mabao 25 wakati Azam ikiwa imefunga mabao 12.

Yanga ina alama 21 baada ya kucheza mechi 11 na ikiwa itashinda mchezo dhidi ya Ndanda unaochezwa leo itashika nafasi ya tatu ikiiacha Mtibwa ambayo ina alama 21 baada ya kucheza mechi 12.

Stand United imemaliza mwaka kwa kushika mkia baada ya kujikusanyia alama saba katika mechi 12 ilizocheza.

Ligi Kuu Tanzania Bara inasimama kwa muda wa wiki mbili kupisha michuano ya Kombe la Mapinduzi ambayo ilianza juzi visiwani Zanzibar

 

African journalist with passion of football reporting.Also i love politics

More in