Connect with us

Simba yanasa straika wa Lusaka Dynamos

Simba yanasa straika wa Lusaka Dynamos

Klabu ya Simba SC ambayo imetangaza kuwa ina dhamira ya kutwaa Kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) kwa miaka ya usoni imeendelea kujiimarisha kwa kufanya usajili wa nyota wa kimataifa.

Baada ya jana kumtambulisha nyota Larry Bwalya wa Zambia leo imetambulisha kumsajili mshambuliaji wa Lusaka Dynamos Chriss Mugalu.

Mugalu ,30, raia wa Congo amejiunga na Simba SC ikiwa haijaweka wazi kiwango cha pesa cha usajili na muda wa mkataba wake huku akitajwa kuwa ujio wake utakuwa umeinarisha safu ya ushambuliaji ya Simba SC inayoongozwa na nahodha John Bocco na Meddie Kagere.

Mugalu aliwahi kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu Zambia 2017 ila mwisho wa mwaka 2019 hakuumaliza vizuri alipata majeraha yaliomuweka nje kwa wiki 12 (miezi 13).

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in