Connect with us

Na Fredrick Nwaka,

Dar es Salaam. Timu za Simba na Yanga zinazotarajiwa kuchuana Jumatano, Agosti 23 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam zitawakisa wachezaji wake muhimu wanaokabiliwa na majeraha.

Yanga itamkosa Obrey Chirwa ambaye hajasafiri kwenda Pemba ilikoweka kambi kwa sababu ya jeraha la kufundo cha mguu.

Mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Tanzania msimu uliopita Mohammed Hussein ‘Shabalala’ pia atashindwa kuichezea Simba katika mchezo dhidi ya Yanga baada ya kuumia katika mechi ya kurafiki dhidi ya Gulioni iliyochezwa Jana usiku mjini Zanzibar.

Timu hizo mbili kubwa nchini, zitakutana ktika mchezo wa ngao ya hisani unaoashiria ufunguzi wa Ligi Kuu msimu wa 2017/18.

Mechi hiyo imekuwa gumzo jijini Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla ambapo mashabiki wa klabu hizo wamekuwa wakitambiana.

More in