Connect with us

Na Fredrick Nwaka,

Dar es Salaam. Miamba ya soka nchini Tanzania Yanga na Simba imeshindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya bao 1-1 katika mchuano wa Ligi Kuu.

Mechi hiyo ilikuwa ya mzunguko wa nane na imechezwa kwenye Uwanja wa Uhuru.

Shiza Kichuya aliifungia Simba bao dakika ya 57 akimalizia makosa ya walinzi wa Yanga kushindwa kuondoa mpira langoni mwao.

Bao la Kichuya lilikuwa la tatu katika michezo ya Simba na Yanga aliyocheza.

Yanga ilisawazisha kupitia Obrey Chirwa dakika ya 60 baada ya walinzi wa Simba kukawia kujisahau kuokoa mpira langoni mwake.

Baada ya mchezo huo mfungaji wa bao la Simba Shiza Kichuya alisema ulikuwa mgumu na matokeo yaliyotokea ni kutokana na makosa ya mchezo huku beki wa Yanga Gadiel Michael akishukuru timu yake kwa kupata bao la kusawazisha

More in East Africa