Connect with us

Simba imeendeleza mwendo wake mzuri wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Singida United.

Mechi hiyo imechezwa kwenye uwanja wa Namfua Mkoani Singida na kuhudhuriwa na maelfu ya mashabiki wa soka kutoka sehemu mbalimbali Tanzania.

Bao la Simba limefungwa na beki wake Shomari Kapombe dakika ya 23 ya mchezo baada ya kutokea purukushani langoni mwa singida United.

Kwa matokeo hayo, ambayo imeshatwaa ubingwa imefikisha alama 68.

Katika mchezo mwingine Kagera Sugar imeishinda Njombe Mji kwa mabao 3-1, mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Kaitaba Mkoani Kagera.

 

African journalist with passion of football reporting.Also i love politics

More in