Connect with us

Klabu ya Simba imefanikiwa kupata tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu wa mwaka 2017/18 baada ya wachezaji wake watatu kuorodheshwa kuwania tuzo hizo.

Wachezaji Erasto Nyoni, John Bocco na Mganda Emanuel Okwi watawania tuzo hiyo katika hafla itakayofanyika Juni 23 mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City Jijini dar es sALAAM.

Nyoni, Bocco na Okwi wamepita katika mchujo ambao awali ulikuwa na wachezaji 30 kutoka klabu mbalimbali.Wachezaji hao walikuwa msaada kwa Simba ulioiwezesha kumaliza ukame wa miaka mitano wa kutoshinda taji la Ligi Kuu.

Majina ya wachezaji hao yamepitishwa na kamati ya tuzo ambapo manahodha wa timu zilizoshiriki ligi hiyo msimu uliopita sambamba na wahariri wa michezo watapiga kura kumchagua mshindi.

Mbali na tuzo ya mchezaji bora, tuzo nyingine 15 zitatolewa katika hafla hiyo zikiwemo mchezaji bora chini ya miaka 20, timu yenye nidhamu, mwamuzi bora, mwamuzi bora msaidizi, kipa bora, kocha bora na goli bora.

Nyingine ni mchezaji wa heshima na kikosi bora kitakachotangazwa siku ya shrehe hizo.

African journalist with passion of football reporting.Also i love politics

More in