Connect with us
Paul Manjale,Dar Es Salaam.
LIGI KUU ya soka ya Vodacom Tanzania Bara maarufu kama VPL inatarajiwa kuendelea tena leo Ijumaa Mei 12, 2017 kwa michezo miwili ya ligi hiyo kubwa nchini kuchezwa katika jiji la Dar Es Salaam.
Katika mchezo wa kwanza mabingwa wa zamani wa ligi hiyo,Simba SC watawaalika Stand United FC ya mkoani Shinyanga kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati katika mchezo wa pili Matajiri wa jiji,Azam FC watakuwa mwenyeji wa Toto Africans ya Mwanza kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, Dar es Salaam.
Ligi hiyo itaendelea tena Jumamosi Mei 13, mwaka huu ambapo JKT Ruvu itakuwa nyumbani Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga kucheza na Majimaji ya Songea wakati Tanzania Prisons itaikaribisha Ndanda ya Mtwara kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya ilihali Mwadui ya Shinyanga itakuwa mgeni wa Mtibwa Sugar Uwanja wa Manungu ulioko Mvomero, Morogoro huku Mbeya City ikisafiri hadi Dar es Salaam kucheza na Young Africans kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Siku ya Jumapili Mei 14, mwaka huu African Lyon ya Dar es Salaam itacheza na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam ilihali siku inayofuata, Jumanne Mei 16, mwaka huu Young Africans tena itakuwa mwenyeji wa Toto Africans kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Funga dimba la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara itakuwa Mei 20,mwaka huu kwa timu zote kucheza ambako Azam FC itakuwa mwenyeji wa Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam wakati Majimaji itamaliza na Mbeya City kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea wakati Simba na Mwadui zitacheza Uwanja wa Taifa,Dar es Salaam.
Siku hiyo Mbao FC itaialika Young Africans ya Dar es Salaam kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza wakati Stand United itamaliza na Ruvu Shooting ya Pwani kwenye Uwanja Kambarage mjini Shinyanga ilihali Mtibwa Sugar itakuwa mwenyeji wa Toto Africans ya Mwanza kwenye Uwanja wa Manungu, Morogoro wakati Africans Lyon ikiwa mgeni wa Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya na Ndanda itamaliza na JKT Ruvu mjini Mtwara kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona.

Ex- CAF Media Expert. An expert on African football with over 15 years experience ,always with an ear to the ground with indepth knowledge of the game. I have worked for top publications including 7 years at www.supersport.com until i founded www.soka25east.com to quench the thirst of football lovers across the continent. I have trained young upcoming journalists who are now a voice in African football.I have covered World Cup,AFCON,CHAN,Champions League,Confederations Cup,Cecafa,Cosafa,Wafu and many other football tournaments across the World. Founder Football Africa Arena(FAA),Founder www.afrisportdigital.com

More in East Africa