Connect with us

Na Fredrick Nwaka,

Dar es Salaam. Timu za Simba na Yanga zimepiga kambi kisiwani Zanzibar kujiandaa na mchezo wa ngao ya hisani.

Yanga itakuwa kiswani Pemba wakati Simba itaweka kambi kisiwani Unguja. Visiwa hivyo viwili vinaunda Zanzibar.

Agosti 23 miamba hiyo ya soka nchini Tanzania itachuana katika Uwanja wa Taifa, mchezo utakaoashiria ufunguzi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu wa 2017/18.

Mechi hiyo tayari imekuwa gumzo miongoni mwa mashabiki wa soka nchini Tanzania kutokana na upinzani uliopp baina ya timu hizo.

Ofisa Mawasiliano wa Simba Haji Manara alisema timu yake itarejea Dar es Salaam siku moja kabla ya mchezo huo.

“Mechi kubwa na muhimu kwetu, hatuengei sana lakini tumepania kuanza vizuri,”alisema Manara.

Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa alisema timu yake imekwenda Pemba kutokana na eneo hilo kuwa mazingira tulivu kwa wachezaji.

“Tumevutiwa na mazingira ya Pemba na tunaamini tutapata wakati mzuri wa kujiandaa,”alisema Mkwasa aliyewahi kuwa mchezaji wa Yanga.

Simba na Yanga ni klabu zenye mashabiki wengi nchini Tanzania.

More in