Connect with us

Ligi Kuu Tanzania Bara inaendelea tena hii leo kwa mchezo mmoja ambapo Singida United inachuana na Simba.

Mchezo huo muhimu kwa Singida United utachezwa katika Uwanja wa Namfua uliopo Mkoani Singida. Singida United inahitaji ushindi ili kushikilia nafasi ya tano.

Simba haina cha kupoteza katika mchezo huo kwa sababu tayari imeshatwaa ubingwa wa ligi kuu baada ya kufikisha alama 65 ambazo haziwezi kufikiwa na timu zote 16 zinazoshiriki Ligi hiyo.

African journalist with passion of football reporting.Also i love politics

More in