Connect with us

Kampuni ya kubashiri mchezo SportPesa, imerejesha ufadhili wa ligi kuu ya soka nchini Kenya KPL.

Mkurugenzi Mkuu wa SportPesa Ronald Karauri amesema kampuni yake itatoa Shilingi Milioni 685 kufadhili soka nchini humo kwa muda wa miaka mitatu ijayo.

Kati ya fedha hizo, Shirikisho la soka FKF, itapata Shilingi Milioni 69 huku ligi kuu KPL ikipangiwa Milioni 259.

Klabu ya Gor Mahia inayoshiriki michuano ya Shirikisho, itapokea Shilingi Milioni 198 huku AFC Leopards ikinufaika na Shilingi Milioni 159.

Hata hivyo, SportPesa haitaendelea na ufadhili wa michezo ya raga na bondia kama ambavyo ilikuwa inafanya hapo awali.

Mwaka uliopita, SportPesa ilijiondoa katika ufadhili wa michezo nchini humo baada ya serikali kuitaka kulipa kodi ya asilimia 35 kutoka kwa mapato inayokusanya kila mwaka.

Hii hatua kubwa kwa maendeleo ya mchezo wa soka nchini humo hasa kwa klabu ya Gor Mahia na AFC Leaoprds ambazo zina historia ndefu ya soka nchini humo.

SportPesa inafadhili pia soka nchini Tanzania hasa llabu ya Simba, Yanga FC na Singida United.

 

More in East Africa