Connect with us

Kampuni ya michezo ya kubahatisha ya Sportpesa inayofadhili vlabu kadhaa kadhaa vya soka nchini Kenya, imetangaza  itasitisha ufadhili wake ifikapo tarehe 1 mwezi Januari mwaka 2018.

Tangazo hili limetolewa na Mkurungenzi Mkuu wa kampuni hiyo Ronald Karauri kupitia ukurasa wake wa Twitter siku ya Ijumaa.

“Kama Sportpesa, tutavifahamisha vlabu na vyama vya michezo tunavyofadhili kwamba tutajiondoa kuanzia tarehe 1 Januari,” alisema Karuri.

Hatua hii imekuja baada ya rais Uhuru Kenyatta kutia saini mswada kuwa sheria, utozwaji ushuru wa faida inayopatikana kutoka kwa kampuni za kubahatisha nchini humo hasa Sportpesa.

Uamuzi wa Sportpesa utakuwa pigo kwa maendeleo ya mchezo wa soka,  raga na masumbwi.

 Sportpesa imetoa ufadhili wa Shilingi za Kenya  Bilioni 1 kufadhili michezo nchini humo.

Vlabu vya soka  vinavyofadhiliwa ni pamoja na AFC Leopards, Gor Mahia na Nakuru All Stars.

More in East Africa