Connect with us

Swahili Stories

Sports Villa kuchuana na Simba mchuano wa kirafiki

Sports Villa kuchuana na Simba mchuano wa kirafiki

Na Victor Abuso

Klabu ya soka kutoka Uganda, Sports Villa imechukua nafasi ya AFC Leopards ya Kenya katika mchuano wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Simba FC ya Tanzania katika siku maalum ya klabu hiyo “Simba Day” mwishoni mwa juma hili jijini Dar es salaam.

Sports Villa imeondoka jijini Kampala siku ya Jumatano kwa usafiri wa barabara kuelekea jijini Dar es salaam kushiriki katika mchuano huo muhimu kwa timu hizo mbili.

Klabu hiyo ya Uganda, ilikuwa Tanzania mwanzoni mwa mwezi uliopita katika mchuano mwingine wa kirafiki na kulazimisha sare ya kutofungana.

Leopards ambayo awali ilikuwa imethibitisha kushiriki katika mchuano huo, haitafika tena Dar es salaam kwa sababu ya mchuano muhimu wa ligi utakaochezwa Jumamosi hiyo dhidi ya Nakuru All Stars, mjini Nakuru.

Simba watatumia mchuano huo wa kirafiki kuwaleta mashabiki wao pamoja lakini pia kutoa nafasi kwa wachezaji wapya waliosajiliwa kuelekea msimu mpya wa soka nchini humo.

Sports Villa nayo inatumia mchuano huu kwa maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu nchini Uganda.

Appointed by CAF President Dr.Ahmad as CAF Media Expert. An expert on African football with over 13 years experience ,always with an ear to the ground with indepth knowledge of the game. I have worked for top publications including 7 years at www.supersport.com until i founded www.soka25east.com to quench the thirst of football lovers across the continent. I have trained young upcoming journalists who are now a voice in African football.I have covered World Cup,AFCON,CHAN,Champions League,Confederations Cup,Cecafa,Cosafa,Wafu and many other football tournaments across the World. Founder Football Africa Arena(FAA),Founder www.afrisportdigital.com

More in Swahili Stories