Connect with us

Taifa Stars inatarajiwa kucheza michezo miwili ya kirafiki katika kalenda ya FIFA inayoanza Machi 19 – 27, 2018 dhidi ya timu za Taifa za Algeria na DR Congo.

Stars itasafiri kuelekea jijini Algiers kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya wenyeji Algeria Machi 22, 2018 na baada ya mchezo huo dhidi ya Algeria, Taifa Stars itarejea nyumbani kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Congo DR Machi 27, 208 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Kocha msaidizi wa Taifa Stars, Hemed Morocco wiki iliyopita alitaja kikosi cha wachezaji wa timu hiyo huku akiwajumuisha wachezaji ambao hawakuwa kikosini kwa muda mrefu akiwemo Thomas Ulimwengu na John Bocco.

Mechi hizi zitakuwa kipimo kwa benchi la ufundi linaloongozwa na Kocha Salum Mayanga ikiwa lina uwezo wa kuivusha Tanzania katika harakati za kuwania kufuzu kucheza fainali za mataifa ya Afrika.

African journalist with passion of football reporting.Also i love politics

More in