Connect with us

Timu ya taifa ya soka ya Sudan Kusini, itamenyana na Uganda katika mzunguko wa pili, kuwania nafasi ya kucheza fainali ya mataifa bingwa barani Afrika kwa wachezaji wanaocheza soka nyumbani CHAN mwaka 2018 nchini Kenya.

Bright Star, ilifuzu katika hatua hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kuishinda Somalia kwa jumla ya mabao 4-1 baada ya mechi zilizochezwa nyumbani na ugenini.

Sudan Kusini wakicheza mjini Djibouti katika uwanja wake wa nyumbani wa Somalia, walipata ushindi wa mabao 2-1, huku wakiwafunga Somalia mabao 2-0 katika uwanja wake wa nyumbani jijini Juba.

Uganda na Sudan Kusini sasa zitamenyana kuanzia mwezi Julai, nyumbani na ugenini. Mshindi atafuzu katika mzunguko wa tatu kutafuta nafasi ya kufuzu katika fainali hiyo ya CHAN.

Mataifa mengine yanayomenyana katika hatua hii ni pamoja na Tanzania wakaomenyana na Rwanda, Djibouti dhidi ya Ethiopia lakini Burundi watakabiliana na Sudan.

Madagascar nao walifuzu baada ya kuishinda Malawi, kwa jumla ya mabao 2-0 na sasa itakabiliana na Msumbiji katika hatua ya pili.

Mauritius ambayo iliishinda Ushelisheli kwa jumla ya mbaoa 3-2, itamenyana na Angola kutafuta nafasi ya kufuzu katika hatua fainali ya CHAN.

More in