Connect with us

 

Wadau wa mchezo wa soka nchini Sudan Kusini wanapiga kura kumchagua rais mpya wa Shirikisho la mchezo huu nchini humo, SSFA.

Aliyekuwa rais Chabur Goc Alei hawanii wadhifa huo baada ya kushindwa kutimiza vigezo vilivyotakiwa ili kuwa mgombea.

Ushindani mkali ni kati ya wagombea watatu, Francis Amin, anayepewa nafasi kubwa ya kuibuka mshindi, Lual Maluk Lual na Arop Joh Aguer.

Wagombea wote wamekuwa wakiahidi kubadilisha usimamizi wa soka nchini humo na kutumia ipasavyo fedha zinazotoka katika Shirikisho la soka duniani FIFA.

Kuelekea katika uchaguzi huu, uongozi wa rais wa zamani umekuwa ukikumbwa na mvutano huku Chabur akishutumiwa kufuja fedha za Shirikisho na hata kulazimika kuondolewa Ofisi kwa nguvu.

Sudan Kusini ambayo inashiriki katika michuano ya kufuzu kucheza soka barani Afrika mwaka 2019 nchini Cameroon, inaorodheshwa katika nafasi ya 147 duniani.

More in