Connect with us

Taifa Stars yaanza mazoezi jijini Dar kuikabili Nigeria

Taifa Stars yaanza mazoezi jijini Dar kuikabili Nigeria

Na Victor Abuso,

Timu ya taifa ya soka ya Tanzania Taifa Stars, imeanza mazoezi katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam kwa maandalizi ya mchuano wao dhidi Nigeria kufuzu katika fainali za mataifa bingwa barani Afrika mwaka 2017 nchini Gabon.

Kocha Charles Mkwasa amesema kikosi chake kitakuwa kinafanya mazoezi mara mbili kwa siku, asubuhi na jioni kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Shirikisho la soka TFF.

Kutokana na kutowepo kwa wachezaji wengi ambao wanajiandaa kwa michuano ya klabu bingwa Tanzania bara msimu huu hasa kutoka vlabu vya Yanga, Simba na Azam FC, kocha Mkwasa ameongeza wachezaji wengine 10 katika kikosi cha taifa.

Wachezaji hao wapya ni pamoja na:- Said Mohamed, Vincent Andrew (wote kutoka Mtibwa Sugar), Mohamed Hussein, Ibrajim Hajibu (Simba SC), Hamis Ali, Juma Mbwana (KMKM), Tumba Sued (Coastal Union), Samuel Kamuntu (JKT Ruvu).

Wengine ni pamoja na, Ibrahim Hilka (Zimamoto-Zanzibar) and Mohamed Yusuf (Prisons), Said Ndemla, Hassan Isihaka, Abdi Banda (wote kutoka Simba SC), Rashid Mandawa (Mwadui FC), Michael Aidan (Ruvu Shooting), Orgeness Mollel (Aspire Academy) na Abdulhaman Mbambi (Mafunzo)

Taifa Stars yaanza mazoezi jijini Dar kuikabili Nigeriaaifa Stars inatarajiwa kuondoka nchini tarehe 23 mwezi Agosti kwenda nchini Uholanzi kwa ziara ya siku 10 kabla ya kurejea nyumbani kuisubiri Super Eagles.

 

Ex- CAF Media Expert. An expert on African football with over 15 years experience ,always with an ear to the ground with indepth knowledge of the game. I have worked for top publications including 7 years at www.supersport.com until i founded www.soka25east.com to quench the thirst of football lovers across the continent. I have trained young upcoming journalists who are now a voice in African football.I have covered World Cup,AFCON,CHAN,Champions League,Confederations Cup,Cecafa,Cosafa,Wafu and many other football tournaments across the World. Founder Football Africa Arena(FAA),Founder www.afrisportdigital.com

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in