Connect with us
Na Fredrick Nwaka,
Dar es Salaam. Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inaendelea na mandalizi ya mchezo muhimu wa kirafiki dhidi ya Botswana.
Mchezo huo utachezwa Septemba 2 kwenye Uwanja wa Uhuru Mjini Dar es Salaam.
Kocha wa timu hiyo Salum Mayanga aliita wachezaji 21 wakiwemo wachezaji saba wanaocheza nje.
Nahodha Mbwana Samatta anayecheza Genk ya Ubelgij na Abdi Banda wa Baroka FC ya Afrika Kusini wameshajiunga kambini.
Simon Msuva wa Al Jadida ya Morocco pia anatarajiwa kuwasili kuanzia leo.
Mazoezi ya Stars yanafanyika katika Uwanja wa Uhuru, utakaotumika kwa mchezo huo baada ya Uwanja wa Taifa kufungwa kwa ajili ya matengenezo

More in African Football