Connect with us

Na Fadhili Omary Sizya,

TIMU ya Mtibwa Sugar imeendeleza ubabe baada ya kuifunga Mbeya City mabao 2-1 Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.

Ushindi huo ni wa pli mfululizo na mabao ya mshambuliaji Stamili Mbonde dakika ya tisa na kiungo Ismail Mhesa dakika ya 42, wakati bao pekee la Mbeya City limefungwa na Erick Kyaruzi dakika ya 48.

Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Tanzania Prisons imeshinda 2-0 dhidi ya Alliance FC Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, mabao ya Laurian Mpalile dakika ya 20 na Ramadhani Ibata dakika ya 85.

Katika Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, bao pekee la mshambuliaji raia wa Burundi, Bigirimana Blaise dakika ya 61 limetosha kuipa pointi tatu Stand United baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Biashara United ya Mara.

Nao Coastal Union wamalazimishwa sare ya 1-1 na KMC ya Dar es Salaam Uwanja wa Mkwakwani Tanga, wenyeji wakitangulia kwa bao la Hamisi Kanduru dakika ya 33 kabla ya Omar Issa kuisawazishia timu ya Manispaa ya Kinondoni dakika ya 79 na Kagera Sugar imetoka sare ya 0-0 na African Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

 

 

More in