Connect with us

By Fadhili Omary Sizya,

 

Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars imeendelea kujifua katika maandalizi ya mchezo wa kimataifa dhidi ya Uganda mechi itakayochezwa septemba 8 2018 kuwania kufuzu fainali za Afcon 2019 nchini Cameroon.

Wachezaji wanaocheza nje ya Tanzania Mbwana Samatta, Ramadhani Kessy, Farid Mussa, Shaban Iddi Chilunda, Thomas Ulimwengu,Abdi Banda, Rashid Mandawa na Simon Msuva wameungana na timu na wapo kwenye mazoezi kwa ajili ya mchezo huo.

Himid Mao anatarajiwa kujiunga leo akitokea Petrojet ya Misri.

Mazoezi kuelekea mchezo huo zikiwa zimebaki siku chache yanafanyika uwanja wa Taifa huku kocha mkuu raia wa Nigeria Emanueli Amunike akiwa na kipindi cha mazoezi asubuhi na jioni ili kujenga haraka uelewano kwa wachezaji hao.

Hali ya kikosi kwa mujibu taarifa ya mwisho wapo katika hali nzuri, kipa namba moja klabuni Simba na Stars Aishi Manula amepona kabisa baada ya kupata maumivu upande wake wa kushoto tangu mchezo wa mwisho ligi kuu bara dhidi ya Mbeya City.

Mchezo huo wa kundi L una uzito mkubwa kutokana na The Cranes kuwa na kikosi imara kwa muda mrefu ikifanikiwa kutikisa ulimwengu wa kandanda Afrika Mashariki na sasa Stars ikinolewa na Amunike ipo katika morali ya kulipa kisasi dhidi ya utawala huo.

Viingilio katika mchezo huo utachezwa uwanja wa Namboole saa 4:00 jioni ni Ordinary Ticket 15,000, V.I.P 40,000 na V.V.I.P 150,000 thamani ya pesa ya Uganda.

 

More in