Connect with us

Tanzania Taifa Stars yalemewa michuano ya Cosafa

Tanzania Taifa Stars yalemewa michuano ya Cosafa

 

Na Victor Abuso,

Timu ya taifa ya soka ya Tanzania, Taifa Stars imebanduliwa nje ya michuano ya COSAFA kuwania taji la kusini mwa nchi za Afrika baada ya kufungwa na Madagascar mabao 2 kwa 0 Jumatano usiku.

 

Tanzania imepoteza mchuano wake wa pili katika michuano hiyo baada ya kufungwa na Swaziland katika mchuano wa ufunguzi kwa bao 1 kwa 0.

 

Madagascar ilipata mabao yake katika dakika ya 14 kupitia mchezaji Rakotoharimalala huku Randrianmanjaka akifunga la pili katika dakika 44 ya kipindi hicho dakika moja kabla ya mapumziko.

 

Mashabiki wa soka nchini Tanzania wamesikitishwa na matokeo hayo hasa kwa kufungwa na Madagascar na Swaziland ambazo zipo chini yake katika orodha ya Shirikisho la soka duniani FIFA.

 

Mwenyekiti wa Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF Jamal Malinzi amesema licha ya kusikitishwa na matokeo hayo, sio mwisho wa soka nchini humo.

 

Kuvunjika koleo sio mwisho wa uhunzi.” alinukuliwa katika ukurasa wake wa Twitter.

 

Vijana wa Stars chini ya kocha Mholanzi Mart Nooij wanasubiri sasa mchuano wake wa mwisho dhidi ya Lesotho kesho Ijumaa kabla ya kurudi jijini Dar es salaam.

 

Wachambuzi wa soka wanasema huenda TFF ikamchukulia hatua kocha Nooij kwa kushindwa kufanya vizuri katika michuano hiyo.

 

Katika matokeo mengine, Swaziland waliwashinda Lesotho mabao 2 kwa 0 na kundi hilo linaoongozwa na Madagascar kwa alama 6 sawa na Swaziland lakini Lesotho na Tanzania hazina alama yoyote.

 

Michuano ya mwisho ya kundi la A zinachezwa leo Alhamisi na mshindi kati ya Zimbabwe na Namibia atafuzu katika hatua ya robo fainali lakini Ushelisheli inaweza kufuzu ikiwa itapata ushindi wa mabao mengi dhidi ya Mauritius ikiwa Zimbabwe itawashinda Namibia.

Ex- CAF Media Expert. An expert on African football with over 15 years experience ,always with an ear to the ground with indepth knowledge of the game. I have worked for top publications including 7 years at www.supersport.com until i founded www.soka25east.com to quench the thirst of football lovers across the continent. I have trained young upcoming journalists who are now a voice in African football.I have covered World Cup,AFCON,CHAN,Champions League,Confederations Cup,Cecafa,Cosafa,Wafu and many other football tournaments across the World. Founder Football Africa Arena(FAA),Founder www.afrisportdigital.com

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in