Connect with us

Tanzania yaanza maandalizi ya kufuzu AFCON 2017 na CHAN 2016

Tanzania yaanza maandalizi ya kufuzu AFCON 2017 na CHAN 2016

Na Victor Abuso,

Timu ya Taifa ya soka ya Tanzania (Taifa Stars) inaingia kambini leo Jumatano jijini Dar es salaam kuanza maandalizi ya mchuano dhidi ya Misri kufuzu katika fainali ya mataifa bingwa barani Afrika AFCON mwaka 2017 nchini Gabon.

Tanzania itaanza safari ya kutafuta tiketi kwenda Gabon ugenini katikati ya mwezi ujao dhidi ya mabingwa hao wa zamani “ Pharao” kabla ya kuwakaribisha Nigeria mwezi Septemba jijini Dar es salaam.

Taifa Stars ambayo ilifuzu katika michuano ya Afrika mara ya mwisho mwaka 1980, imejumuishwa katika kundi moja na Nigeria, Misri na Chad.

Kocha Mart Nooij aliyepewa nafasi nyingine na uongozi wa TFF kuhakikisha kuwa Tanzania inafanya vizuri katika michuano ijayo hasa kufuzu katika michezo ya CHAN itakayofanyika mwakani nchini Rwanda tayari amewaita wachezaji kwa maandalizi ya michuano hiyo.

Nooij, amewaita wachezaji 16 kuingia kambini na kitu cha kwanza kinachofanyika siku ya Jumatano ni kwa wachezaji hao kupimwa afya zao na kujua maandeleo yao kabla ya kuwajumisha katika kikosi cha pamoja kitakachokua kwenye maandalizi ya mchezo dhidi ya Misri.

Wachezaji walioitwa kuingia kambini ni pamoja na , Mohamed Hussein, Peter Manyika, Hassan Isihaka, Jonas Mkude (Simba SC), Salum Telela, Juma Abdul, Nadir Haroub (Yanga SC), Aishi Manula, Mudathir Yahya, Frank Domayo, Kelvin Friday (Azam FC), Rashid Mandawa, Atupele Green (Kagera Sugar), Haroun Chanongo (Stand United) Malimi Busungu (Mgambo JKT) na Emmanuel Simwanda (African Lyon).

Mara baada ya kurejea kutoka nchini Afrika Kusini, kocha wa Stars Nooij aliwapa mapumziko ya siku 10, wachezaji waliokua kwenye michuano ya Cosafa mpaka Juni Mosi ambapo ndipo watajumuika na wachezaji wengine waliopo kambini.

Ifikapo Juni Mosi, 2015 Taifa Stars itaanza kambi ya moja kwa moja kujiandaa na mechi dhidi ya Misri itakayochezwa jijini Alexandria katika uwanja wa Borg El Arab Juni 14, 2015 ikiwajumuisha pia wachezaji Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaocheza soka la kulipwa katika klabu ya TP Mazembe ya Congo DR.

Kabla ya kuelekea nchini Misri, Taifa Stars inatarajiwa kuweka kambi jijini Addis Ababa nchini Ethiopia kuanzia tarehe 4,Juni 2015 kwa muda wa wiki moja kabla ya kuelekea nchini Misri kwenye mchezo huo dhidi ya Mafarao.

Juni 20, 2015 Taifa Stars itawakaribisha Uganda kwenye uwanja wa Amani mjini Zanzibar katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN, zitakazofanyika nchini Rwanda 2016, na mchezo wa marudiano kufanyika baada ya wiki mbili nchini Uganda.

Ex- CAF Media Expert. An expert on African football with over 15 years experience ,always with an ear to the ground with indepth knowledge of the game. I have worked for top publications including 7 years at www.supersport.com until i founded www.soka25east.com to quench the thirst of football lovers across the continent. I have trained young upcoming journalists who are now a voice in African football.I have covered World Cup,AFCON,CHAN,Champions League,Confederations Cup,Cecafa,Cosafa,Wafu and many other football tournaments across the World. Founder Football Africa Arena(FAA),Founder www.afrisportdigital.com

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in