Connect with us

Televisheni ya taifa nchini Tunisia Wataniya, imetishia kuacha kuonesha mechi zote za ligi kuu ya  soka nchini humo baada ya wanahabari wake wawili kujeruhiwa mwishon mwa wiki iliyopita baada ya kushambuliwa na mashabiki.

 Mashabiki wa klabu ya Etoile du Sahel walivamia eneo la matangazo ya kituo hicho ambayo ina haki ya kuonesha ligi ya soka nchini Tunisia.

Mbali na wanahabari hao kujeruhiwa, mitambo ya Televisheni hiyo iliharibiwa baada ya mashabiki waliokuwa na hasira  kuvamia eneo la utangazaji baada ya klabu yao kufungwa na Club Africain bao 1-0.

Mzozo ulianza kipindi cha pili, baada ya Club Africain ilipozawadiwa penalti uamuzi ambao uliwakasirisha mashabiki wa Etoile du Sahel.

Hii sio mara ya kwanza kwa wanahabari wa kituo hicho cha taifa kuvamiwa wakati wa michuano ya soka nchi humo na wanataka wafanyikazi wao kupewa ulinzi la sivyo, wataacha kuonesha mechi hizo za soka.

Mwezi Februari, maafisa wa polisi 38 walijeruhiwa baada ya mashabiki kuanza kupigana wakati wa mchuano wa wapinzani wa jadi Etoile du Sahel na  Esperance de Tunis.

Waziri wa michezo Majdouline Cherni ameelezea kinachoendelea kushuhudiwa uwanjani nchini humo kama  ugaidi uwanjani.

More in North African Football