Connect with us

TFF kutoa mafunzo kwa waamuzi

TFF kutoa mafunzo kwa waamuzi

Na Victor Abuso

Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF, litatoa mafunzo kwa waamuzi wake wanaochezesha mechi za ligi kuu na zile za daraja la kwanza kwa maandalizi ya kuanza kwa msimu mpya wa soka mwaka huu.

Msemaji wa TFF, Baraka Kizuguto amesema mafunzo hayo yatafanyika jijini Dar es salaam kati ya tarehe 21 hadi 24 mwezi Agosti.

Kizuguto amesisitiza kuwa mafunzo hayo yatatolewa kwa waamuzi watakaochezesha mechi za msimu huu wala hayatakuwa kwa waamuzi wote.

Waamuzi hao ni sharti wawe na umri wa kati ya miaka 21 hadi 45 kwa wanawake huku kwa wanaume umri wa chini ukiwa wa miaka 23 na ule wa juu ukiwa wa 45 na watahitaji kuwasilisha vyeti vya kuzaliwa kabla ya kuanza mafunzo hayo.

Pamoja na mafunzo ya darasani, waamuzi hao pia watalazimika kufanya mtihani wa mazoezi na pia watafanyiwa uchunguzi wa kiafya.

Marefarii 40 na manaibu wao 70 wanatarajiwa kushiriki katika mafunzo hayo.

Ex- CAF Media Expert. An expert on African football with over 15 years experience ,always with an ear to the ground with indepth knowledge of the game. I have worked for top publications including 7 years at www.supersport.com until i founded www.soka25east.com to quench the thirst of football lovers across the continent. I have trained young upcoming journalists who are now a voice in African football.I have covered World Cup,AFCON,CHAN,Champions League,Confederations Cup,Cecafa,Cosafa,Wafu and many other football tournaments across the World. Founder Football Africa Arena(FAA),Founder www.afrisportdigital.com

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in