Connect with us

TFF kutoa tuzo kwa wachezaj bora wa ligi kuu msimu huu

TFF kutoa tuzo kwa wachezaj bora wa ligi kuu msimu huu

Na Victor Abuso

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kwa kushirikiana na wadhamini wa Ligi Kuu kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom, kesho siku ya alhamis tarehe wanatarajia kutoa zawadi kwa washindi wa ligi kuu ya soka msimu huu.

Hafla hiyo imeratibiwa kufanyika jijini Dar es salaam na mgeni rasmi atakuwa ni Juma Nkamia, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

Vodacom watatoa zawadi kwa Bingwa wa Ligi Kuu msimu 2014/2015, mshindi wa pili, mshindi wa tatu na mshindi wa nne, baadhi ya vipengele vitakavyotolewa zawadi pia na wadhamini hao wa Ligi Kuu ni :

1. Mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
Mohamed Hussein (Simba SC)
Mrisho Ngasa (Young Africans)
Saimon Msuva (Young Africans)

2. Mlinda mlango bora wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
Mohamed Yusuph (Tanzania Prisons)
Said Mohamed (Mtibwa Sugar)
Shaban Hassan (Coastal union)

3. Kocha bora wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
Goran Kopunovic (Simba SC)
Hans Van Der Pluijm (Young Africans)
Mbwana Makata – (Tanzania Prisons)

4. Mwamuzi bora wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
Israel Mjuni Nkongo
Jonesia Rukyaa
Samwel Mpenzu

5. Timu yenye nidhamu Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
Mgambo JKT
Mtibwa Sugar
Simba SC

MAHUNDI MCHEZAJI BORA MWEZI MEI
Wakati huo huo mchezaji John Mahundi wa timu ya Coastal Union amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Mei, 2015 na jopo la makocha kufuatia kuwazidi wachezaji wengine 14 aliokuwa anananiwa nao nafasi hiyo.

Kwa kuibuka mchezaji bora wa mwezi mei, Mahundi atazawadiwa fedha taslimu Shilingi za Kitanzania milioni moja (1,000,000) kutoka kwa wadhamini wa Ligi Kuu kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom.

Ex- CAF Media Expert. An expert on African football with over 15 years experience ,always with an ear to the ground with indepth knowledge of the game. I have worked for top publications including 7 years at www.supersport.com until i founded www.soka25east.com to quench the thirst of football lovers across the continent. I have trained young upcoming journalists who are now a voice in African football.I have covered World Cup,AFCON,CHAN,Champions League,Confederations Cup,Cecafa,Cosafa,Wafu and many other football tournaments across the World. Founder Football Africa Arena(FAA),Founder www.afrisportdigital.com

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in