Connect with us

Na Fredrick Nwaka,

Dar es Salaam. Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF) linaomboleza msiba wa aliyewahi kuwa katibu mtendaji wa Chama cha Soka Tanzania (FAT) Chabanga Hassan Dyamwale.

Mbali na kuwa katibu mtendaji wa FAT, Dyamwale pia aliwahi kushika wadhifa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii katika utawala wa Serikali ya rais Julius Nyerere.

Kiongozi huyo alifariki dunia jana na anatarajia kuzikwa Mkoani Tanga, Kaskazini Mashariki wa Tanzania.

Katika salamu zake za pole kwa familia Karia ameelezea kuguswa na msiba huo.

“Alikuwa mtu makini na muhimu aliyeatanguliza mbele maslahi ya soka la Tanzania, ametoa mchango mkubwa ambao hautasahaulika,”aamesema Karia,aliyechaguliwa jumamosi kuwa rais wa TFF

More in East Africa