African Football

TFF yamteua Salum Mayanga kocha mpya wa Taifa Stars

on

 

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limemteua Salum Mayanga kuwa kocha wa muda wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’.

Kocha Salum Mayanga anachukua nafasi ya Kocha Charles Boniface Mkwasa ambaye mkataba wake unafikia mwisho mwezi Machi, mwaka huu wa 2017.

TFF inasema kocha Mayanga atakuwa na kazi ya kuandaa kikosi cha timu ya Taifa kwa ajili ya hatua ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika 2019.

Michuano hiyo ya awali kwenda nchini Cameoon, inatarajiwa kuanza mapema mwaka huu.

Aidha, kocha Mayanga atakuwa na kibarua cha kukiandaa kikosi cha wachezaji wanaocheza soka nyumbani, kufuzu kucheza fainali ya taji la CHAN mwaka ujao nchini Kenya.

Kocha Mkwasa, alipewa kazi ya kuifunza Tanzania baada ya kufutwa kazi kwa Mart Nooij kocha kutoka Uholanzi mwaka 2015 kwa sababu ya matokeo mabaya.

About Victor Abuso

You must be logged in to post a comment Login