Connect with us
Na Fredrick Nwaka,
Mzunguko wa nane wa Ligi Kuu Tanzania Bara unatamatika leo lakini kivumbi kinaonekana kwa timu nne za ambazo zina alama 16.
Simba, Yanga, Mtibwa na Azam zote zina alama 16 zikishika nafasi nne za juu.
Simba inakaa kileleni ikiwana idadi ya magoli mengi ya kufunga, magoli 20.
Yanga ina mabao 11 ikiwa nafasi ya pili, Mtibwa Sugar iko nafasi ya tatu na imefunga mabao saba.
Azam inashika nafasi ya nne ambayo licha ya kuwa na alama 16 lakini ina mabao 6.
Tanzania prisons na Ruvu Shooting Leo zinakamilisha mzunguko wa nane kwa kuchuana na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Sokoine Mkoani Mbeya.
Wakati huohuo, Kagera Sugar ilipata ushindi wake wa kwanza Jana kwa kuichapa Ndanda FC mabao 2-1.
Ligi hiyo itaendelea mwishoni mwa wiki hii kwa michezo ya mzunguko wa tisaa

More in