Connect with us

Timu za Taifa zaanza maandalizi ya michuano za kufuzu AFCON 2017

Timu za Taifa zaanza maandalizi ya michuano za kufuzu AFCON 2017

Na Victor Abuso,

Timu mbalimbali za taifa za mchezo wa soka katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na kwingineko barani Afrika zinashuka dimbani mwishoni mwa juma hili kujipima nguvu katika michuano ya Kimataifa ya kirafiki.

Mataifa ya Afrika yanatumia michuano hii kujiandaa kwa mechi za kwanza kuwania nafasi ya kucheza katika fainali za kombe la mataifa bingwa barani Afrika mwaka 2017 nchini Gabon.

Siku ya Jumamosi, Kenya itamenyana na Tanzania jijini Kigai nchini Rwanda , huku Amavubi Stars nao wakiwa nyumbani watapambana na Sudan Kusini katika mchuano mwingine.

Niger watakabiliana na Gabon jijini Niamey, huku Guinea wakimaliza kazi na Chad.

Siku ya Jumapili, Ethiopia itaikaribisha Zambia huku Mali ikipepetana na Libya.

Mechi za kwanza zitapigwa kuanzia mwishoni mwa juma lijalo. Tanzania ambao wamejumuishwa katika kundi moja na Nigeria, Misri na Chad, wataanza kampeni zake dhidi ya mabingwa wa zamani Misri ugenini.

Kocha wa Taifa Stars Mholanzi Mart Nooij ameahidi kufanya vizuri katika michuano hiyo na kufuzu Gabon baada ya matokeo mabaya katika michuano iliyopita ya COSAFA baina ya mataifa ya Kusini mwa Afrika.

Kenya nayo inayofunzwa na kocha wa zamani wa Uganda Cranes Bobby Williamson, itaanza ugenini dhidi ya Congo Brazaville.

Mbali na Congo, Kenya imejumuishwa pia na Guinea Bissau na Zambia.

Uganda itaanza kazi na Bostwana katika kundi ambalo pia lina Burkina Faso na Comoros.

Rwanda nayo imepangwa na Ghana, Msumbiji na Mauritius na itaanza mchuano wake dhidi Msumbiji.

Leopard ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ipo katika kundi moja na Angola, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Madagascar.

Ex- CAF Media Expert. An expert on African football with over 15 years experience ,always with an ear to the ground with indepth knowledge of the game. I have worked for top publications including 7 years at www.supersport.com until i founded www.soka25east.com to quench the thirst of football lovers across the continent. I have trained young upcoming journalists who are now a voice in African football.I have covered World Cup,AFCON,CHAN,Champions League,Confederations Cup,Cecafa,Cosafa,Wafu and many other football tournaments across the World. Founder Football Africa Arena(FAA),Founder www.afrisportdigital.com

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in