Connect with us

TP Mazembe njiani kunyakua ubingwa wa Afrika

TP Mazembe njiani kunyakua ubingwa wa Afrika

Klabu ya soka ya TP Mazembe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, siku ya Jumamosi ilianza vema safari ya kutwaa ubingwa wa taji la klabu bingwa barani Afrika msimu huu wa mwaka 2015.

Mazembe wakicheza ugenini walipata ushindi muhimu dhidi ya USM Alger mabao 2 kwa 1 nchini Algeria.

Mchezaji wa kimataifa wa Zambia, Ranford Kalaba alikuwa wa kwanza kuipa timu yake baola ufunguzi lakini baadaye akapata adhabu ya kupewa kadi nyekundu.

Mazembe ambao ni mabingwa wa mwaka 2010 wana nafasi kubwa ya kunyakua tena taji hili ikiwa watapata sare au kupata ushindi Jumapili ijayo katika fainali ya mwisho mjini Lubumbashi.

Licha ya penalti yake kuokolewa na kipa wa USM Alger, Mtanzania Mbwana Samatta alitikisa nyavu ya wapinzani hao na kuiongezea ushindi klabu yake.

USM Alger walipata bao la kufuta machozi katika dakika za lala salama kabla ya mchuano huo kumalizika.

Takwimu kamili:

USM Alger 1 – 2 TP Mazembe

Waliofunga mabao: Rainford Kalaba (28’), Mbwana Samatta (77’) for TP Mazembe; Mohamed Seguer (88’) for USMA

Kikosi cha USM Alger: Zemmamouche, Benayada, Boudebouda, Mazari, Khoualed, El Orfi, Ferhat, Koudri, Nadji, Beldjilali, Benmoussa

Kikosi cha TP Mazembe: Kidiaba, Frimpong, Kimwaki, Coulibaly, Boateng, Diarra, Sinkala, Kalaba, Ulimwengu, Samatta, Traore

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in