Connect with us

Klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imefuzu katika hatua ya fainali, kuwania taji la Shirikisho barani Afrika.

Mabingwa hao watetezi walifuzu katika hatua hiyo licha ya kutofungana na FUS Rabat ya Morocco katika nusu fainali ya pili uliopigwa usiku wa kuamkia leo.

Mazembe walifanikiwa kwa sababu, walikuwa wamepata ushindi wa bao 1-0 wiki kadhaa zilizopita mjini Lubumbashi.

Wawakilishi hawa wa DRC sasa wanasubiri mshindi wa nusu fainali ya pili kati ya SuperSport United ya Afrika Kusini na Club Africain ya Tunisia.

Mechi hiyo inachezwa baadaye siku ya Jumapili, na timu zote mbili zinakwenda katika mchuano huu baada ya sare ya bao 1-1.

Wydad Casablanca ya Morocco nayo, imefuzu katika hatua ya fainali kuwania taji la klabu bingwa baada ya kuishinda USM Alger ya Algeria kwa jumla ya mabao 3-1.

Nusu fainali ya kwanza, timu zote mbili hazikufungana.

Wawakilishi hao wa Morocco sasa wanasubiri mshindi kati ya Etoile du Sahel ya Tunisia dhidi ya Al-Ahly ya Misri katika nusu fainali ya pili.

Mchuano wa kwanza wa nusu fainali, Etoile du Sahel walishinda mabao 2-1.

More in African Football