Connect with us

 

TP Mazembe ya DRC ambao ni mabingwa watetezi wa taji la Shirikisho barani Afrika wamefanikiwa kufuzu katika hatua ya makundi baada ya mchuano wake wa mwishoni mwa juma lililopita.

Licha ya kutoka sare ya 0-0 dhidi ya JS Kabylie ya Algeria, imefuzu kwa sababu ya ushindi wa mabao 2-0 katika mchuano wa kwanza wiki mbili zilizopita mjini Lubumbashi.

Haya ni matokeo mazuri kwa Mazembe ambao wanataka kutetea taji hili baada ya kuondolewa katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika.

Klabu hii yenye makao yake mjini Lubumbashi pia imekuwa ikabiliwa na changamoto ya kuwa na kocha baada ya kochawake  kutoka Ufaransa Thierry Froger kufutwa kazi mwezi Machi.

Mbali na TP Mazembe, vlabu vingine ambavyo vimefuzu katika hatua ya makundi ni pamoja na:-

MC Alger-Algeria

Recreativo do Libolo-Angola

Smouha-Misri

CF Mounana-Gabon

Horoya-Guinea

FUS Rabat-Rabat

Platinum Stars-Afrika Kusini

SuperSport United-Afrika Kusini

Al-Hilal -Sudan

Mbabane Swallows-Swaziland

Club Africain-Tunisia

CS Sfaxien-Tunisia

KCCA-Uganda

ZESCO United-Zambia

Klabu moja inasubiriwa kati ya Rivers Unites ya Nigeria na Rayon Sport ya Rwanda kufuzu katika hatua hii. Mchuano wa kwanza, Rivers walishinda kwa mabao 2-0 huku mchuano wa marudiano ukirajiwa kuchezwa siku ya Jumamosi jijini Kigali.

Droo ya hatua ya makundi, itafanyika tarehe 26.

Kutakuwa na makundi manne, kila kundi na timu nne.

Mshindi na yule wa pili, wote watafuzu katika hatua ya robo fainali.

 

More in