Connect with us

TP Mazembe yafuzu hatua ya makundi

TP Mazembe yafuzu hatua ya makundi

 

Klabu ya soka ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, imefanikiwa kufuzu katika hatua ya hatua kuwania taji la Shirikisho barani Afrika.

Mazembe imefuzu katika hatua hiyo licha ya kufungwa mabao 2 kwa 1 na Stade Gabesien ya Tunisia siku ya Jumanne jioni.

Klabu hiyo kutoka mjini Lubumbashi ilifuzu kwa sababu ya bao la ugenini la bao 1 kwa 0 na hivyo bao la ugenini liliwasaidia kusonga mbele.

Youssef Fouzai aliifungia penalti klabu yake katika dakika ya 38 kipindi cha kwanza lakini Jonathan Bolingi akaizawazishia Mazembe lakini Ahmed Hosni akairejesha kileleni Stade Gabesien.

Hata hivyo, Esperance de Tunis iliondolewa katika michuano hiyo baada ya kutoka sare ya bao 1 kwa 1 na Mouloudia Bejaia ya Algeria.

Mchuano wa kwanza ulitoka sare ya kutofungana katika mchuano wa kwanza.

Ratiba ya leoo na matokeo ya mzunguko wa kwanza:-

  • Stade Malien (Mali) vs FUS Rabat (Morroco) 0-0
  • Etoile du Sahel (Tunisia) vs CF Mounana (Gabon) 2-0
  • Al-Ahli Tripoli (Libya) vs Misr Lel Makkasa (Misri) 0-0
  • Al-Merrikh (Sudan) vs Kawkab Marrakech( Morroco) 1-0
  • Young Africans (Tanzania) vs Sagrada Esperanca (Angola) 2-0
  • Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini) vs Medeama (Ghana) 3-1

Timu nane zitafuzu katika hatua ya makundi.

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in