Connect with us

Nahodha wa Azam Himid Mao amesema timu yake inarudi kwa nguvu katika Ligi Kuu baada ya kutwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi.

Azam ilishinda taji la pili mfululizo la michuano hiyo baada ya kuishinda URA kwa penati 4-3 baada ya timu hizo kutoka sare ya bila kufungana katika muda wa dakika 90.

Akizungumza na soka25east, Mao ambaye alifunga penati moja katika mchezo huo amesema wachezaji wa timu hiyo wana ari kubwa kuhakikisha Azam inavuna alama nyingi na mwisho wa msimu kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu.

“Ubingwa wa Mapinduzi umetupatia hamasa kubwa, kila mchezaji ana hamu ya kutoa mchango mkubwa kwa timu ili tupate matokeo na kupanda juu ya msimamo,”alisema mchezaji huyo ambaye pia huichezea timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.

Azam inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na alama 26 sawa na Simba lakini imezidiwa idadi ya magoli ya kufunga na kufungwa.

Azam imefungwa mabao 12 na kufungwa mabao matatu wakati Simba imefungwa mabao 25 na kufungwa mabao sita.

African journalist with passion of football reporting.Also i love politics

More in