Connect with us

Twiga Stars kujipima nguvu na Harambee Starlets

Twiga Stars kujipima nguvu na Harambee Starlets

Na:Victor Abuso,

Timu ya Taifa ya soka ya Tanzania ya Wanawake Twiga Stars, inatarajiwa kucheza na timu ya taifa ya Kenya, Harambee Starlets katika mchuano wa Kimataifa wa kirafiki tarehe 23 mwezi huu.

Mchuano huu utachezwa katika uwanja wa Amaan Kisiwani Zanzibar katika maandalizi ya kujiandaa kwa fainali za michezo ya Afrika itakayofanyika nchini Congo Brazaville mwezi ujao.

Twiga Stars inaendelea na mazoezi mara mbili kwa siku katika uwanja wa Amaan chini ya kocha Rogasian Kaijage ikiisubiri Harambee Starlets.

Tanzania imepangwa kundi moja na Nigeria, Ghana na wenyeji Congo Brazaville.

Twiga Stars ilifuzu katika michuano hii baada ya kuindoa Zambia kwa mabao 6 kwa 5 katika michuano ya kufuzu katika michuano hiyo.

Kikosi cha Starlets ni :Fatuma Omari, Belina Julius, Happiness Hezron, Fatuma Hassan, Anastazia Anthony, Fatuma Bashiru, Fatuma Issa, Fatuma Khatibu, Maimuna Hamis, Donizia Daniel, Sofia Mwasikili, Etoe Mlenzi.


Wenigine ni Amina Ally, Thereza Yonna, Mwanahamisi Omari, Stumai Abdallah, Shelder Boniface, Asha Rashid, Najiat Abbas, Estha Chabruma, Mwajuma Abdallah na Fatuma Mustapa

Starlets ya Kenya ilitolewa na Banyana Banyana ya Afrika Kusini katika michuano ya kufuzu kwa michezo ya Olimpiki itakayofanyika nchini Brazil mwaka ujao.

 

Ex- CAF Media Expert. An expert on African football with over 15 years experience ,always with an ear to the ground with indepth knowledge of the game. I have worked for top publications including 7 years at www.supersport.com until i founded www.soka25east.com to quench the thirst of football lovers across the continent. I have trained young upcoming journalists who are now a voice in African football.I have covered World Cup,AFCON,CHAN,Champions League,Confederations Cup,Cecafa,Cosafa,Wafu and many other football tournaments across the World. Founder Football Africa Arena(FAA),Founder www.afrisportdigital.com

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in