Connect with us

Uchambuzi :Hatima ya CAF baada ya Kujiuzulu kwa Rais Sepp Blatter

Uchambuzi :Hatima ya CAF baada ya Kujiuzulu kwa Rais Sepp Blatter

Na Victor Abuso,

Uamuzi wa Joseph Sepp Blatter kutangaza kujiuzulu kuwa rais wa Shirikisho la soka duniani FIFA siku chache tu baada ya kuchaguliwa umeushangaza ulimwengu wa soka hasa bara la Afrika na Asia waliompigia kura kwa wingi.

Hata kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa mwezi uliopita, viongozi wa Afrika walitangaza kwa kauli moja kuwa watampigia kura Blatter ili aendelee kuongoza soka duniani.

Amaju Pinnick rais wa Shirikisho la soka nchini Nigeria NFF alinukuliwa akisema kuwa Blatter ndiye mtu wa pekee ambaye amehakikisha kuwa Afrika inapata maendeleo ya soka.

Hatuwezi kuamini mtu ambaye anatuahidi kutufanyia kazi, tutamchagua Blatter kwa sababu tumeona yale aliyotufanyia,” Pinnick alisisitiza.

Rais wa Shirikisho la soka barani Afrika Issa Hayatou alionekana mwenye furaha kubwa baada ya Blatter kushinda na hata baada ya hotuba yake, viongozi wa soka barani Afrika na Mataifa ya Caribbean walimzingira Blatter na kumpongeza kwa kupata ushindi.

Je, kujiuzulu kwa Blatter mwenye umri wa miaka 79 kunaashiria mabadiliko ya soka pia barani Afrika ? Je, wakati wa Hayatou ambaye ambaye amekuwa uongozini tangu mwaka 1986 inafikia ukingoni ? Haya ni maswala yanayoendelea kuulizwa lakini tukirejelea suala la Blatter ni kwanini ajiuzulu wakati huu ?

Kwanini alijizulu wakati huu

Shinikizo kutoka kwa maafisa wa Shirika la ujasusi la FBI kuwachunguza maafisa saba waliokamatwa kwa tuhma za ufisadi zimemkosesha usingizi.

Ripoti zinasema kuwa tayari FBI wameanza kumchungua Blatter ikiwa anahusika kwa namna yoyote na tuhma hizo ?

Blatter amesema hawezi kuendelea kuongoza FIFA kwa sababu haungwi mkono na kila mmoja.

Ameahidi mabadiliko makubwa kabla ya kuondoka rasmi mwezi Desemba au kabla ya mwezi Machi mwaka ujao.

Nani anaweza kumrithi Blatter ?

Ni swali ambalo kila mmoja anajiuliza. Wachambuzi wa soka wanasema FIFA inasema mtu ambaye ataweza kuliunganisha tena Shirikisho hilo baada ya kuonekana kugawanyika wakati wa uongozi wa Blatter.

Suala lingine kuu la kujizuliza je, wale waliompigia kura watafanya hivyo kwa yule atakayependelewa na Blatter ikiwa atafanya hivyo ?

Rais wa Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA Michel Plattini ni miongoni mwa watu wanaopewa kipau mble kuwania nafasi hii, lakini ikiwa atafanya hivyo itamlazimu atafute mbinu za kupata kura kutoka nje ya bara la Ulaya.

Mtu mwingine ni Mwanamfalme wa Jordan Hussein Bin Ali aliyepambana na Blatter katika uchaguzi uliopita na kushindwa.

Jeffrey Webb, ambaye pia alionekana kuwa katika nafasi nzuri ya kuwania wadhifa huo baada ya Blatter inavyoonekana hatafanya hivyo kwa sababu ni mmoja wa washukiwa wa ufisadi .

Nini hali ya baadaye ya FIFA ?

Mkuu wa idara ya kuhakikisha kuwa kanuni za FIFA zinaheshimiwa Domenico Scala, amesema kwa sasa Shirikisho hilo linahitaji mabadliko makubwa.

Changamoto ni kwamba mabadiliko yoyote ni lazima yapigiwe kura na wajumbe wa Fifa kutoka kote duniani hali ambalo tumeshuhudia wakati mwingine yakipingwa.

Hata hivyo shinikizo hizi za ufisaidi kutoka kwa FBI na wafadhili mfano kampuni ya Cocacola huenda yakaleta mabadiliko.

Scala pia anasema mabadiliko muhimu ni kuwepo kwa mihula ya kuhudumu katika shirikisho hilo, kwa sasa hakuna muda maalum wa rais wa FIFA kumaliza muda wake.

Mfano Blatter amekuwa katika uongozi wa FIFA kwa miaka 17.

Pamoja na hayo, huenda pia ikiwa wajumbe watapitisha kwa mara ya kwanza, mshahara wa rais wa FIFA utawekwa wazi.

 

Ex- CAF Media Expert. An expert on African football with over 15 years experience ,always with an ear to the ground with indepth knowledge of the game. I have worked for top publications including 7 years at www.supersport.com until i founded www.soka25east.com to quench the thirst of football lovers across the continent. I have trained young upcoming journalists who are now a voice in African football.I have covered World Cup,AFCON,CHAN,Champions League,Confederations Cup,Cecafa,Cosafa,Wafu and many other football tournaments across the World. Founder Football Africa Arena(FAA),Founder www.afrisportdigital.com

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in