Connect with us

Uchambuzi: TP Mazembe ililemewa hatua ya robo fainali kombe la dunia

Uchambuzi: TP Mazembe ililemewa hatua ya robo fainali kombe la dunia

Kumekuwa na hisia mseto nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya TP Mazembe kufungwa katika hatua ya robo fainali kuwania ubingwa wa kombe la dunia baina ya vlabu.

Baadhi ya mashabiki wanahisi kuwa maanadalizi ya TP Mazembe hayakuwa mazuri kuelekea michuano hiyo huku wengine wakidokeza kuwa ilikuwa ni tu bahati mbaya kwa timu yao kufungwa.

Mchambuzi wa soka na mwandishi wa Habari wa AFP Lucien Kahozi Koshia ameiambia soka25east.com akiwa mjini Osaka kuwa, wachezaji wa Mazembe walilemewa na kasi ya Sanfrecce Hiroshima.

Mazembe walionesha mchezo mzuri katika mechi zilizopita lakini pia katika mchuano wa robo fainali na licha ya kupata kona saba walishindwa kutumia nafasi hizo kupata ushindi.

Wachezaji wa Mazembe wanaotoka nchi nane barani Afrika hawakuwa na mazoezi ya pamoja, hali ya hewa ilikuwa nzuri hapa Japan lakini Mazembe walilemewa,” alisema Kahozi.

Aidha, kwa mujibu wa Kahozi kutokuwepo kwa kipa wa siku nyingi na mwenye uzoefu mkubwa Robert Kidiaba, huenda kulichangia Mazembe kufungwa.

Naamini kama Kidiaba angekuwa langoni, mambo yangekuwa tofauti.Kidiaba hapa Japan walikuwa wanamwongopa sana na hata nilishuhudia jezi yake ikiteketezwa moto,” aliongeza Kahozi.

TP Mazembe sasa itachuana na Cub America ya Mexico siku ya Jumatano kutafuta mshindi wa nafasi ya tano katika mashindano hayo.

Mapema siku ya Jumapili, Club America ilipoteza katika hatua ya robo fainali baada ya kufungwa na Guangzhou Evergrande ya China kwa mabao 2 kwa 1.

Michuano ya nusu fainali ni siku ya Alhamisi, Barcelona watachuana na Guangzhou Evergrande ya China huku Sanfrecce Hiroshima  ya  Japan ikichuana River Plate kutoka Argetina.

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in