Connect with us

Kocha wa timu ya taifa ya Uganda Mfaransa Sebastien Desabre amekitaja kikosi cha mwisho cha wachezaji 23, kinachojiandaa kushiriki katika fainali ya michuano ya CHAN kwa wachezaji wanaocheza soka nyumbani nchini Morocco siku ya Jumapili.

Kikosi hiki cha mwisho kimekuja baada ya Uganda kupoteza mchuano wake wa Kimataifa wa kirafiki dhidi ya Congo Brazaville mjini Rabat na kufungwa bao 1-0.

Wachezaji wawili waliochwa nje katika kikosi hicho Mustapha Kizza beki wa klabu ya KCCA na kiungo wa kati Tom Masiko kutoka klabu ya Vipers, wanarejea nyumbani jijini Kampala.

Kikosi kamili:

Makipa: Isma Watenga (Vipers Sc), Benjamin Ochan (KCCA FC), Saidi Keni (Proline FC)

Mabeki: Nico Wakiro Wadada (Vipers Sc), Joseph Nsubuga (Sc Villa Jogoo), Isaac Muleme (KCCA FC), Aggrey Madoi (Police FC), Timothy Dennis Awanyi (KCCA FC), Bernard Muwanga (Sc Villa Jogoo),  Mujuzi Mustapha (Proline FC)

Viungo wa Kati: Tadeo Lwanga (Vipers SC), Ibrahim Saddam Juma (KCCA FC), Muzamiru Mutyaba (KCCA FC), Milton Karisa (Vipers SC),  Abubaker Kasule (Express FC), Allan Kyambadde (SC Villa Jogoo), Paul Mucureezi (KCCA FC), Rahmat Senfuka (Police F.C)

Washambuliaji: Derrick Nsibambi (KCCA FC), Muhammad Shaban (KCCA FC), Nelson Senkatuka (Bright Stars FC)

 

Maafisa wa kiufundi:

  • Mkuu wa msafara: Hamid Juma (FUFA Mjumbe wa Kamati Kuu FUFA)
  • Kocha: Sebastien Desabre
  • Kocha msaidizi: Mathias Lule

Ratiba ya Uganda, (Kundi B)

  • Uganda v Zambia – Januari 14 2018 (Marrakech)
  • Uganda v Namibia – Januari 18 2018 (Marrakech)
  • Uganda v Ivory Coast – Januari 22 2018 (Marrakech)

Ratiba ya michuano ya ufunguzi:-

Kundi A: Morocco, Guinea, Sudan na Mauritania

Januari 13 2018:- Morocco v Mauritania

Januari 14 2018:-Guinea v Sudan

Kundi B: Ivory Coast, Zambia, Uganda na Namibia

Januari 14 2018:-Ivory Coast v Namibia

Januari 14 2018:-Zambia v Uganda

Kundi C: Libya,Nigeria, Rwanda na Equitorial Guinea

Januari 15 2018: Libya v Equitorial Guinea

Januari 15 2018: Nigeria v Rwanda

Kundi D: Angola, Cameroon, Congo na Burkina Faso

Januari 16 2018: Angola v Burkina Faso

Januari 16 2018: Cameroon v Congo

More in African Football