Connect with us

Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, yameanza kwa kusuasua katika mzunguko wa pili wa michuano ya kufuzu kucheza fainali ya vijana wasiozidi miaka 20 katika mchezo wa soka mwaka 2019 nchini Niger.

Tanzania ilianza vibaya ikicheza nyumbani siku ya Jumapili, baada ya kufungwa na Mali kwa mabao 2-1.

Mambo yalikuwa vivyo hivyo dhidi ya Rwanda, baada ya kufungwa na Zambia 2-0.

Burundi nayo ikicheza nyumbani, ilitoka sare ya bao 1-1 na Sudan.

Hata hivyo, Uganda ilianza vema baada ya kuifunga Cameroon bao 1-0 jijini Kampala.

Michuano ya marudiano ni mwishoni mwa juma lijalo.Washindi watafuzu katika hatua ya tatu.

Timu 16 bora zitacheza nyumbani na ugenini mwezi Julai huku mshindi akifuzu katika fainali hiyo.

More in African Football