Connect with us

Timu ya taifa ya soka ya Uganda jioni hii wameifunga Misri bao 1-0 katika mchuano muhimu wa kufuzu kucheza fainali ya kombe la dunia mwaka ujao nchini Urusi.

Bao la ushindi lilitiwa kimyani na mshambuliaji Emmanuel Okwi katika kipindi cha pili cha mchuano huo.

Matokeo haya yamewapa furaha kubwa maelfu ya mashabiki wa soka waliofurika katiuka uwaja wa Naambole jijini Kampala.

Ushindi huu wa Uganda inayofunzwa na kocha wa nyumbani Moses Basena, inaifanya kuongoza katika kundi E kwa alama 7 baada ya mechi tatu, huku ikifuatwa na Misri ikiwa na alama 6.

Timu hizi mbili zitakutana tena tarehe tano mwezi ujao mjini Alexandria.

Ghana na Congo Brazzavile watamenyana Ijumaa katika mechi nyingine ya kufuzu katika fainali hii.

Guinea na Libya nao wanamenyana leo katika mchuano mwingine wa kundi A.

Ijumaa Septemba 1 2017

  • Tunisia vs DR Congo
  • Nigeria vs Cameroon
  • Morocco vs Mali
  • Cape Verde vs Afrika Kusini

More in East Africa