Connect with us

Shirikisho la soka duniani, FIFA, limetangaza viwango vya ubora siku ya Alhamisi kuelekea kombe la dunia wiki ijayo nchini Urusi.

Ujerumani inaendelea kuongoza duniani, ikifuatwa na Brazil.

Ubelgiji ipo katika nafasi ya tatu, Ureno ya nne huku Argentina ikifunga tano bora.

Barani Afrika, Tunisia ni ya kwanza lakini ya 21 dunia. Senegal ni ya pili  barani Afrika huku DRC ikiwa ya tatu na ya 38 duniani.

Uganda ni ya 82 duniani baada ya kushuka nafasi nane, huku Kenya ikiwa ya 112 duniani.

Rwanda 136, Tanzania 140, Burundi 148.

More in African Football