Connect with us

Ujumbe wa Samatta kwa Watanzania wanaodai amecheza chini ya kiwango dhidi ya Libya

Ujumbe wa Samatta kwa Watanzania wanaodai amecheza chini ya kiwango dhidi ya Libya

Na Mwandishi wetu akiwa Dar Es Salaam,

Baada ya baadhi ya watanzania mitandaoni kumshishia lawama nahodha wa timu yao ya Taifa Mbwana Samatta kufuatia kupoteza mchezo kwa  kufungwa 2-1 dhidi ya Libya mchezo wa kuwania kufuzu kucheza fainali za mataifa ya Afrika (AFCON 2021).

Mbwana Samatta ,26, anayekipiga katika klabu ya KRC Genk ameweka wazi mawazo yake na namna alivyopokea tuhuma hizo kuhusiana ma kudaiwa mchezo huo alicheza chini ya kiwango, huku wengine wakidai kuwa Samatta hajitoi Taifa Stars kwa kiasi kikubwa kama ilivyokuwa KRC Genk.

“Nimepata meseji na comment kutoka kwa watu kadhaa kuwa awajaelewa kiwango nilichoonesha ktk mechi za timu ya taifa, anyway ukweli nimefurahi kuona watu wanasema ukweli sichukulii binafsi bali nachukulia km chachu itakayonifanya nijitume zaidi ili niweze Bora zaidi, HAINA KUFELI” aliandika Samatta kupitia ukurasa wake wa twitter

Mchezo wa Libya na Tanzania ulimalizika kwa Tanzania kupoteza 2-1, Libya wakitokea nyuma huku Mbwana Samatta akifunga goli la Tanzania dakika ya 18 kwa mkwaju wa penati iliyopatikana baada ya Saimon Msuva kuchezea madhambi katika eneo la 18, Tanzania sasa inakuwa nafasi ya tatu katika Kundi J lenye timu za Tunisia mwenye alama 6, Libya nafasi ya pili kwa kuwa na alama 3 sawa na Tanzania ila ushindi dhidi ya Tanzania unamuweka juu (head to head) na Equatorial Guinea akiendelea kuburuza mkia kwa vipigo viwili mfululizo.

CHAN 2020 MATCHES

Must See

More in