Connect with us

Beki wa klabu ya Standard Liège nchini Ubelgiji Merveille Bope Bokadi, hatakuwepo katika kikosi cha timu yake ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kitakapomenyana na Libya katika mchuano muhimu wa kufuzu kucheza kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi.

Bokadi atakosa mchuano huyo kwa sababu ana jeraha ambalo litachukua wiki kadhaa kupona.

Mchuano huu utachezwa katika uwanja wa Mustapa Ben Jannet mjini Monastir nchini Tunisia.

Libya inachezea mechi zake za nyumbani nchini Tunisia kwa sababu ya hali ya kiusalama katika nchi yao.

Wakati huo Leopard iliwasili mjini Casablanca, nchini Morocco kujiandaa kumenyana na Libya.

Baada ya kocha Jean-Florent Ibenge kuwataja wachezaji wake 23, kikosi chake kimelazimika kusalia na wachezaji 22 baada ya jeraha la Bope.

Leopard inakwenda katika mchuano huu ikiwa katika nafasi ya pili kwa alama saba nyuma ya Tunisia ambayo ina alama 10.

Guinea na Libya tayari hazina nafasi ya kufuzu katika fainali hiyo.

Kikosi kamili cha DRC:

Makipa:

 1. Matampi Vumi Ley (TP Mazembe)
 2. Joël Kiasumbua (Lugano/Uswizi)
 3. Nathan Mabruki (Daring Club Motema Pembe)

Mabeki:

 1. Issama Mepko (TP Mazembe)
 2. Gabriel Zakuani (Gilligam/Uingereza)
 3. Marcel Tisserand (Wolfsburg/Uingereza)
 4. Fabrice Nsakala (Alanyaspor/Tunisia)
 5. Glody Ngonda Muzinga (Vita Club)
 6. Christian Luyindama Nekadio (Standard de Liège/Ubelgiji
 7. Wilfried Moke (Konyaspor/Tunisia)

Viungo wa Kati:

 1. Chancel Mbemba (Newcastle/Uingereza)
 2. Chikito Lema Mabidi (Raja Casablanca/ Morocco)
 3. Neeskens Kebano (Fulham/Uingereza)
 4. Paul-José Mpoku (Standard de Liège/Ubelgiji)
 5. Gaël Kakuta (Amiens/Ufaransa)

Washambuliaji:-

 1. Jordan Botaka (Saint-Trond/Ubelgiji)
 2. Cédric Bakambu (Villareal/Uhispania)
 3. Firmin Mubele (Rennes/Ufaransa)
 4. Jonathan Bolingi (Mouscron/Ubelgiji)
 5. Junior Kabananga (FK Astana/Kazakhstan)
 6. Chadrack Akolo (VBF Stuttgart/Ujerumani)
 7. Arnold Nkufo Isako (Sélubal/ Ureno

More in African Football